1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

 | 03.12.2008 | 15:00 UTC

Kikosi cha Umoja wa Ulaya cha kupambana na uharamia kuchukuwa nafasi ya kikosi cha NATO

BRUSSELS

                   Kikosi cha majini cha Umoja wa Ulaya kitachukuwa nafasi ya meli za kivita za kikosi cha Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO kupambana na maharamia nje ya fukwe za Somalia.

                   Waziri wa mambo yas nje wa Ujerumani Frank Walter- Steinmeir ameunga mkono kuwepo kwa kikosi hicho cha manowari cha Umoja wa Ulaya kwa kusema kwamba kinahitajika kulinda meli kwa kutumia vikosi vya kimataifa.Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinatazamiwa kutowa meli kwa ajili ya kikosi hicho wakati pia Ufaransa na Italia zitatowa ndege.

                 Makabidhiano ya opresheni hiyo yamepangwa kufanyka tarehe 15 mwezi wa Desemba.

               Wakati huo huo maharamia wa Somalia wameiachilia huru meli ya Yemen waliokuwa wameiteka juma lililopita baada ya mazungumzo yaliofanikiwa kati ya maafisa wa kanda,wazee wa kikabila na watekaji nyara wa meli hiyo.

                 Inaelezwa kwamba meli hiyo imeachiliwa bila ya kulipwa fedha za kuigombowa.



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Journal (deutsch) - Mit Tagesthema