1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

 | 03.12.2008 | 15:00 UTC

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice yuko India kutuliza uhusiano kati ya nchi hiyo na Pakistan

NEW DELHI

                Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice aishinikiza Pakistan kuchukuwa hatua haraka kusaidia uchunguzi wote wa India kuwatia mbaroni wahusika wa mashambulizi ya mji wa Mumbai ambayo yametishia uhusiano kati ya India na Pakistan.

              Rice amesema Pakistan inatakiwa kuchukuwa hatua haraka na kwa nia kutowa ushirkiano wake kikamilifu na kwa uwazi.Rice ametowa kauli yake hiyo leo hii mjini New Delhi wakati akiwa ziarani nchini India.

   Rice alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa India Pranab Mukherjee na Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh.Rice ambaye hapo kesho anatarajiwa kwenda Pakistan amesema ujumbe huo utawasilishwa kwa Pakistan.

           Rice yuko nchini India kujaribu kutuliza uhusiano ulioachafuka kati ya India na Pakistan kutokana na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya mji wa Mumbai nchini India yaliouwa watu zaidi ya 171.

            Waziri Mkuu wa Pakistan Asif Ali Zardari amegoma kuwapeleka nchini India watuhumiwa 20 waliotajwa na India na kusema watafunguliwa mashtaka nchini Pakistan baada ya serikali ya India kuwasilisha ushahidi madhubuti.l

    



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Kick off! Report - Kick off! Report