1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages


 

Matukio ya Kisiasa | 19.03.2010

Wabunge wa Ujerumani waipitisha bajeti

 

Wabunge wa Ujerumani leo wameipitisha bajeti ya waziri wa fedha Wolfgang Schäuble.

 

Wabunge wa Ujerumani leo wameipitisha bajeti ya mwaka huu wa fedha,jumla ya Euro Bilioni 320,lakini wajumbe wa vyama vya upinzani wameilaumu serikali kwa kukusudia kuongeza denila nchi hadi Euro bilioni 82.

Waziri wa fedha wa Ujerumani,Wolfgang Schäuble,leo amesisitiza ulazima wa kurejea katika njia ya matumizi bora ya fedha ili kukabiliana na deni hilo.

Akizungumza bungeni,kuchangia katika mjadala wa bajeti ya Ujerumani kwa mwaka mpya wa  fedha, waziri Schäuble ametangaza mpango kabambe utakaowezesha kuziweka sawa hesabu za fedha mnamo miaka inayofuata .

Waziri huyo amesema lazima Ujerumani irejee katika njia ya matumizi bora ya fedha ili kuweza kuziweka sawa hesabu za nchi.

Wabunge wa Ujerumani wameipitisha bajeti hiyo ya Euro Bilioni 320, lakini serikali inatarajiwa kuongeza deni kwa Euro Bilioni 82. Kiwango hicho hakijawahi kufikiwa katika historia ya Ujerumani.

Hata hivyo,waziri wa fedha Schäuble amesema bidii kubwa zitafanywa ili kulipunguza deni hilo hatua kwa hatua .

Katika bajeti ya mwaka huu,kiasi cha Euro Bilioni 319 kitatengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mapato ya yanatarajiwa kufikia kiasi cha Euro Bilioni 211.

Serikali pia itatenga kiasi cha Euro Bilioni 28 kwa ajili ya kuekeza katika vitega uchumi. Wabunge wa vyama vya upinzani wameilamu serikali kwa mpango wa kuongeza deni

Hapo awali,kiongozi wa wabunge wa chama cha SDP, Frank- Walter Steinmeier,amesema walipa kodi sasa watalipa kwa niaba  ya mawakala wa  ulanguzi na mabenki yenye uchu wa faida.

Wabunge 313 walipiga kura kuipitisha bajeti hiyo na 256  waliipinga.

Mwandishi Mtullya Abdu/DPA/ZA

Mhariri: Miraji Othman

         

          

 

 

Abdu Said Mtullya

 

Send us an e-mail »Send »Print »

More on the topic

 
Share this article


 
Wafanyakazi
Waliochutama kutoka kushoto: Sekione Kitojo,Halima Nyanza,Josephat Charo na Ramadhani Ali. Waliosimama kutoka Kushoto: Susanne Bergers-Rose,Abdul Mtullya,Saumu Mwasimba,Mohamed Abdulrahman,Othman Miraji, Andrea Schmidt,Thelma Mwadzaya, Mohamed Dahman,Oumilkher Hamidou,Samia Othman na Nina Markgraf

DW-TV EUROPE live

Im Focus

We're sorry, due to legal issues this content can not be transmitted as live stream.

If you are inside the United States, it is still possible for you to enjoy DW-TV. For more information, please click here.

Global Media Forum
Global Media Forum
SHINDANO JIPYA LA IDHAA YA KISWAHILI
Simu ya mkononi, zawadi mojawapo kwa washindi
Kiswahili On Your Desktop via RSS
RSS